Wednesday, September 26, 2012

THOMAS MLAMBO WA SUPER SPORTS ATUA NCHINI KURUSHA LIVE KWA MARA YA KWANZA NCHINI KIPINDI CHA "SOCCER AFRICA"... ATAKUWA PAMOJA NA WACHAMBUZI MAARUFU WA SOKA BARANI AFRIKA; MAMADOU NA TK...!

Thomas Mlambo


Mamadou Gaye

Thojmas Mlambo (kushoto) na Mamadou Gaye (wa pili kushoto) wakiwa kazini.
Mchambuzi wa soka  TK wa Super Sport akiwa na straika Asamoah Gyan
Mtangazaji Thomas Mlambo wa kituo cha televisheni cya kulipia cha DSTV ametua nchini kurusha 'live' kwa mara ya kwanza kesho kipindi cha "Soccer Africa" kupitia chaneli yao ya Super Sport 3.

Mlambo atarusha kipindi hicho na wachambuzi maarufu wa soka barani Afrika, ambao ni Mamadou Gaye na TK.

Afisa Habari wa kampuni ya Multi Choice (Tanzania), Barbara Kambogi, ambao kampuni yao mama ya Afrika Kusini ndiyo inayomiliki DSTV, amesema leo kuwa kipindi hicho kitarushwa live kesho kuanzia saa 4:30 usiku kwenye hoteli ya Sunrise jijini Dar es Salaam.

"Huu ni mwanzo tu wa kuelekea kurusha mechi za Ligi Kuu ya Bara kupitia chaneli zetu za Super Sport... Watanzania wajiandae kupata burudani nzuri zaidi," amesema Barbara.

Msimu huu, Super Sport watarusha kwa majaribio baadhi ya mechi kali za Ligi Kuu ya Bara, ikiwamo ile itakayowakutanisha mahasimu wa jadi Simba na Yanga itakayochezwa Oktoba 3 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment