Wednesday, September 26, 2012

EVRA: HAMNA MWENYE UHAKIKA WA NAMBA MAN UTD


BEKI wa kushoto wa Manchester United, Patrice Evra (31) amesema hakuna mchezaji yeyote aliye na uhakika wa namba kwenye kikosi chao msimu huu.


------------------------------------------

RIO KUKAUSHIWA TIMU YA TAIFA ENGLAND


ROY Hodgson hatarajiwi kumrejesha beki Rio Ferdinand (33) kwenye timu ya taifa ya England licha ya John Terry (31) kustaafu kuichezea taifa.


------------------------------------------

WALCOTT: NAMMISI RVP


WINGA wa Arsenal, Theo Walcott amekiri kwamba alijisikia vibaya sana kumuona Robin van Persie akiondoka Manchester United. 


Walcott amesema alikuwa karibu sana na Mholanzi huyo.

"Daima unawamisi wachezaji bora na yeye ni rafiki mkubwa na mweledi wa uhakika. Namtakia mema Manchester United. Daima alikuwa akinitafuta na kunisapoti. Nammisi sana lakini unapaswa kusahau na kusonga mbele." 


 ------------------------------------------

MOURINHO NITAFUNDISHA HADI MIAKA 70 KAMA FERGIE


KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema amedhamiria kufundisha soka kwa miaka mingi kama Sir Alex Ferguson.

 Mourinho ni rafiki mzuri wa kocha huyo wa Manchester United.

"Najua vyema kwanini Alex bado anafanya kazi katika umri ule nadhani nitafanya kama hivyo. Napenda soka na napenda kufundisha. Nitakuwa bado mdogo wakati nitakapofikisha miaka 50 (Januari mwakani) na nina mengi mbele yangu," alitabasamu Mourinho.
 

------------------------------------------

ALVES: NEYMAR NJOO BARCA


DANIEL Alves amesapoti mpango wa Barcelona kutaka kumsajili nyota wa Santos, Neymar.

Barca wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Brazil.

"Natamani siku moja kuja kuwaona Neymar na (Lionel) Messi pamoja uwanjani. Atafaa vyema vyama. Barca watakuwa na wachezaji wawili bora duniani," alisema Alves. (Marca)
 

------------------------------------------

RAMOS HAENDI MAN CITY


BEKI wa Real Madrid, Sergio Ramos (26) hatajiunga na Manchester City hivi karibuni baada ya kumalizatofauti zake na kocha wa Real, Jose Mourinho.

Ramos ametwaa ubingwa wa La Liga mara tatu akiwa na Real Madrid.
------------------------------------------

LLORENTE AONGEA INTERWAWAKILISHI wa mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Fernando Llorente wako katika mazungumzo na Inter Milan.

Gazeti la Tuttosport limesema kaka wa Llorente amesafiri kwenda Milan kuzungumza na Inter kuhusu uhamisho wa Januari.

Mkataba wa Llorente unamalizika Juni.
------------------------------------------FRIMPONG KUREJEA ARSENAL LEO USIKU

KIUNGO wa Arsenal, Emmanuel Frimpong (20) anatarajiwa kurejea kikosini leo usiku katika mechi ya Kombe la Ligi ambalo sasa linaitwa Capital One Cup dhidi ya Coventry baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi saba kutokana na majeraha.

No comments:

Post a Comment