Monday, September 17, 2012

SZCZESNY AUMIA TENA... AACHWA KATIKA KIKOSI CHA ARSENAL KITAKACHOCHEZA LEO DHIDI YA MONTPELLIER KATIKA MECHI YA UFUNGUZI LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA

Wojciech Szczesny
LONDON, England
Kipa Wojciech Szczesny atakosa mechi ya klabu yake ya Arsenal katika ufunguzi wa Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Montpellier itakayochezwa kesho Jumanne kutokana na jeraha la enka.

Kipa huyo wa kimataifa wa Poland atarithiwa nafasi yake na Muitalia Vito Mannone katika mechi hiyo dhidi ya mabingwa wa Ligue 1 (Ligi Kuu ya Ufaransa), klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imesema leo katika taarifa  iliyotolewa kupitia tovuti yao (www.arsenal.com).

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa Szczesny bado alikuwa ndiye chaguo lao la kwanza licha ya kufanya makosa Jumamosi yaliyowazawadia goli Southampton katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England waliyoshinda 6-1.

"Wojciech ndiye namba moja hadi hapo nitakapobadili mawazo yangu," amesema Mfaransa Wenger.

No comments:

Post a Comment