Monday, September 17, 2012

DAVID SILVA ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MITANO KUENDELEA KUICHEZEA KLABU MANCHESTER CITY

David Silva
MANCHESTER, England
KIUNGO David Silva ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia na pia mshindi mara mbili wa fainali za Euro, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake ya Manchester City inayoshikilia ubingwa wa Ligi Kuu ya England, klabu hiyo imesema leo.

Kiungo huyo mchezeshaji wa Hispania, aliyetua Man City akitokea Valencia Julai 2010, amesema kwamba mipango ya Man City ndiyo iliyomvutia kaisi cha kukubali kusaini mkataba huo mrefu.

"Timu inakua na sasa tumepania kutwaa taji la Liagi ya Klabu Bingwa Ulaya na hiyo ni sababu nyingine inayonifanya intake kubaki hapa na kujaribu kutwaa kila taji," amesema Silva kupitia tovuti ya klabu yao (www.mcfc.co.uk).

No comments:

Post a Comment