Monday, September 17, 2012

PIPI: MWANANGU KINGSTONE NIMEMZAA NA MUME WANGU... TULIOANA WAKATI MIMBA IKIWA YA MIEZI NANE ...!

Pipi katika pozi kali kabla ya kupata mtoto.
Huyui ndiye Kingstone... mtoto wa Pipi
Pipi
Pipi
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Pipi, amesema kuwa mtoto wake wa kiume Kingstone ambaye alijifungua hivi karibuni, amempata kutoka kwa mumewe halali.

Pipi amefichua hayo leo wakati akizungumza kupitia mahojiano yake yaliyorushwa kwenye kipindi cha Bongo Amplifanya kinachorushwa na redio ya Clouds FM.

Msanii huyo mwenye miaka 20, alisema kuwa alishaoana kimila na mzazi mwenzie wakati mimba ya mwanawe (Kingstone) ilipofikisha miezi nane.

"Kimila tuko ndani ya ndoa... tulioana wakati mimba yangu ina miezi 8," amesema Pipi ambaye stori yake ilishika nafasi ya sita katika 'top 10' za leo.

Pipi ni msanii aliyejizolea umaarufu kwa kuimba nyimbo za "kubembeleza", na hivi karibuni alikamilisha albamu ya nyimbo 10 akiwashirikisha wakali kama Jua Cali, Gnako na Mangwear.

No comments:

Post a Comment