Friday, September 21, 2012

SIMBA, YANGA WAFURAHIA MABASI YAO MAPYA KUTOKA KILIMANJARO PREMIUM LAGER

Mabasi mapya aina ya Yutong waliyokabidhiwa kwa klabu za Simba na Yanga leo na wadhamini wao kampuni ya bia nchini (TBL) kupitia bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kama sehemu ya udhamini wao wa Sh. bilioni 5 kwa miaka mitano. Mabasi hayo yenye siti 50 ikiwamo maalum ya kukaa kocha ama nahodha na nyingine moja ya dereva, yana thamani ya Sh. milioni 450.
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (kulia) akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro


Soka si uadui.... Mashabiki wa Simba na Yanga wakishangilia pamoja wakati wa sherehe za timu zao kukabidhiwa mabasi mapya kutoka kwa wadhamini wao kampuni ya TBL kupitia bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager

Kulia Rage akijadili na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL

Rage akimuonyesha kipengele tata Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah

Dole la Rage katika kipengele tata
Sanga akikabidhiana makabrasha ya basi na Mkurugenzi wa TBL


Rage akibadilishana makabrasha na Mkurugenzi wa TBL
Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa kushoto akisaini kabrasha
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akikabidhiwa mfano wa ufunguo
Clement Sanga akikabidhiwa mfano wa ufunguo
PICHA ZOTE: www.Bongostaz.blogspot.comNo comments:

Post a Comment