Friday, September 21, 2012

ARSENAL WAMEKUWA WAKALI ZAIDI BILA YA VAN PERSIE - MANCINI

Roberto Mancini
Straika Robin van Persie wa Manchester United akikokota "ngoma" wakati wa mechi yao ya Kundi H la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini  Manchester, England Septemba 19, 2012. Man U walishinda 1-0.
Kiungo Alex Song wa Barcelona akikimbia na mpira wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Valencia kwenye Uwanja wa Nou Camp mjini Barcelona, Hispania Septemba 2, 2012.
Kiungo Santi Cazorla wa Arsenal akishangilia goli ka pili la timu yake wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, England  Septemba 2, 2012.
Straika Lukas Podolski wa Arsenal (katikati) akishangilia goli lake wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Montpellier Herault kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Ufaransa Septemba 18, 2012.

Straika Olivier Giroud wa Arsenal akijiuliza wakati wa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Montpellier Herault kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Ufaransa Septemba 18, 2012.

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini kwamba Arsenal wanatisha zaidi msimu huu katika mbio za ubingwa licha ya kuwapoteza nyota wao wakubwa katika kipindi kilichoisha cha usajili.

Nahodha na straika wao Robin van Persie na kiungo wao wa ulinzi Alex Song waliondoka Emirates Stadium na kujiunga na klabu za Manchester United na Barcelona lakini Mancini anaona kwamba wakali kama Lukas Podolski, Santi Cazorla na Olivier Giroud waliojiunga katika kikosi cha Arsene Wenger wameifanya timu hiyo kuwa kali zaidi.

"Arsenal anaweza kupigania ubingwa msimu huu," Mancini aliwaambia wanahabari kuelekea mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu ya England baina ya timu hizo mbili.

"Wamekuwa bora zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita, licha ya kwamba wamewapoteza wachezaji wao bora. Pengine, kwa sababu hiyo, presha imepungua kwao msimu huu.

"Wamempoteza Van Persie na Song, lakini wachezaji waliowanunua wameleta uzoefu na ubora kikosini."

No comments:

Post a Comment