Sunday, September 16, 2012

MASHABIKI 112 TU WASHUHUDIA MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING


WATAZAMAJI 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema leo kuwa mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa Sh. 3,000 na Sh. 10,000 ni Sh. 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu Sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja Sh. 100,000 na tiketi Sh. 89,916.

Kamati ya Ligi Sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh. 3,928.78, gharama za mchezo Sh. 9,821.95 na uwanja Sh. 9,821.95.

No comments:

Post a Comment