Thursday, September 20, 2012

SHAKIRA: NINA UJAUZITO WA GERARD PIQUE

Gerard Pique akijiachia na Shakira
Gerard Pique akijiachia na Shakira
Gerard Pique akijiachia na Shakira
Mmmmnywaaah! I love yuu soo 'macho' baby..... Gerard Pique akila bata na Shakira ufukweni

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique anajiandaa kuwa baba kwa mara ya kwanza.

Mchumba wake nyota wa pop, Shakira ametangaza kwamba ana ujauzito wa nyota huyo wa Hispania.

"Kama ambavyo baadhi yenu mnafahamu, Gerard na mimi tunasubiri kwa hamu ujio wa mtoto wetu wa kwanza! Tumeamua kutoa nafasi kwa jambo hili kubwa maishani kwetu na kusitisha mambo mengine yote ya ziada tuliyopanga katika siku za karibuni.

"Napenda kuwashukuru mashabiki wangu kwa upendo wao wa daina na kunielewa.

"Busu kubwa!

"Na tutaona punde!

"Shakira"

No comments:

Post a Comment