Thursday, September 20, 2012

REAL MADRID MAMBO BADO SI MAMBO, CASILLAS HAKUSHANGILIA GOLI LA RONALDO

Iker Casillas aliuchuna hakushangilia goli la Ronaldo

Cristiano Ronaldo akishangilia kwa kuteleza kwa magoti baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Manchester City katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid juzi. Real ilishinda 3-2.
Mourinho naye alipagawa, alishangilia kwa kuteleza kwa magoti kama Ronaldo baada ya straika huyo kufunga goli la ushindi dhidi ya Manchester City katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid juzi. Real ilishinda 3-2.
Cristiano Ronaldo pamoja na Marcelo baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Manchester City katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid juzi. Real ilishinda 3-2.

Wachezaji wote walikuwa na furaha isipokuwa Casillas

Kwa wachezaji, mashabiki hadi kocha Mourinho ilikuwa ni raha tupu... vipi kuhusu Casillas?

MAHUSIANO baina ya nahodha wa Real Madrid, Iker Casillas na Cristiano Ronaldo kwa mara nyingine yamezua maswali baada ya ushindi dhidi ya Manchester City.

Goli la dakika za lala salama la Ronaldo, lililowapa ushindi wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, liliwafanya mashabiki, wachezaji na kila mmoja wa timu hiyo  kuwehuka kwa furaha huku kocha Jose Mourinho akishangilia kwa kuteleza kwa magoti utadhani mchezaji.

Hata hivyo, Casillas hakuhusika katika sherehe hizo, huku kituo cha televisheni cha TVE kikibainisha video inayomuonyesha kipa huyo akiwa hashangilii, wala hata kuonyesha ishara yoyote ya kusapoti wakati uwanja ukilipuka kwa furaha.

No comments:

Post a Comment