Sunday, September 23, 2012

RVP KAFUATA PESA MAN UTD - LEHMANN

Van Magoli
Kipa Jens Lehmann na Manuel Almunia akianglia jambo kabla ya kuanza kwa mechi yao ya Ligi Kuu ya England baina ya Arsenal na  Blackburn Rovers kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, Aprili 2, 2011.

Jens Lehmann akiokoa hatari kutoka kwa DJ Campbell wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya England baina ya Arsenal na Blackpool kwenye Uwanja wa Bloomfield Road mjini Blackpool, England Aprili 10, 2011.
Jens Lehmann akiwa uwanjani wa kati wa mechi ya ligi kuu ya England baina ya Arsenal na Blackpool kwenye Uwanja wa Bloomfield Road mjini Blackpool, England Aprili 10, 2011.

Zilipendwa.... Makipa Jens Lehmann na Manuel Almunia "wakipasha" kabla ya kuanza kwa mechi yao ya Ligi Kuu ya England baina ya Arsenal na  Blackburn Rovers kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, Aprili 2, 2011.

SHUJAA wa Arsenal, Jens Lehmann anaona kwamba kuuzwa kwa Robin van Persie kwenye klabu ya Manchester United yalikuwa ni maamuzi sahihi.

Lehmann anaamini kwamba Arsenal waliwaonyesha uwajibikaji katika kipindi cha uhamisho.

Aliliambia gazeti la Sunday Mirror: "Unapomuangalia Robin van Persie - mchezaji anataka kuondoka kwa ajili ya kufuata pesa na pengine kwa sababu anadhani kwamba mahala kwingine bi rahisi kushinda, unapaswa kumuacha aondoke, hasa anapokuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake, na anapokuwa amecheza msimu mmoja bila ya majeraha katika miaka nane ama tisa, hilo ni jambo la kushangaza kwa Robin. Na mwisho unajiuliza tubaki naye ama tumuuze?

"Hivyo muda utatuambia, na nini kitafuata mwakani itakapokuja kanuni ya UEFA ya kudhibiti matumizi makubwa ya fedha (financial fair play). Hapo ndipo tutakapoona ikakavyokuwa kwa klabu kama Chelsea, Man City, ambao wanatumia fedha nyingi zaidi ya bajeti zao na kisha kugeukia kwa Arsenal kuwa juu ya klabu zote hizo."

No comments:

Post a Comment