![]() |
Torres |
KOCHA wa Chelsea, Roberto di Matteo amekerwa na maoni yaliyotolewa na Ruud Gullit kuhusu Fernando Torres.
Kocha wa zamani wa Chelsea, Gullit, ambaye alimsajili Di Matteo Stamford Bridge mwaka 1996, aliponda kufuatia kiwango kibovu kilichoonyeshwa na Torres dhidi ya Juventus Jumatano kwa "isingekuwa jambo baya" kama anguumia kwa sababu kwa wakati ule walikuwa "wakicheza watu 10".
Gullit aliongeza: "Nimeanza kuchoshwa na huyu jamaa (Torres). Hayumo mchezoni. Hayupo katika maeneo anayopaswa kuwepo. Anachofanya hakitoshi. Kwa mchezaji wa kiwango chake, nataka zaidi kutoka kwake.
"Hayumo mchezo kabisa. Najaribu kujiuliza ana matatizo gani huyu."
Lakini Di Matteo alijibu: "Tunamfurahia.
"hata asipofunga anatengenezea wenzake nafasi za kufunga na anafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya timu na daima ana mchango kwetu.
"Kwa wakti huu hatuna tatizo. Kubadili mfumo wa uchezaji si jambo tunalojadili kwa sasa. Tunaye mshambuliaji na tunamfurahia.
"Tunatarajia Daniel Sturridge atapona na kurejea haraka. Kwa sasa mfumo wetu ni kumchezesha straika mmoja."
No comments:
Post a Comment