Saturday, September 15, 2012

REAL MADRID YAINGIZA 'MIHELA' YA AJABU... NI REKODI YA AINA YAKE ISIYOWAHI KUFIKIWA NA KLABU YOYOTE YA SOKA NA PIA ZA MICHEZO MINGINE YOTE DUNIANI....!

Kikosi cha Real Madrid 2012-13
MADRID, Hispania
Real Madrid imefunga mwaka wake wa fedha 2011-12 kwa 'kicheko' baada ya kuvuna mapato ya euro milioni 514 (Sh. trilioni 1.033), ambayo ni ongezeko la asilimia saba kulinganisha na mwaka wa fedha uliopita.

Kiasi hiki ni rekodi ya aina yake duniani kwani hakuna timu nyingine ya mchezo wowote ule duniani, achilia mbali soka, iliyowahi kuingiza fedha hizo na Real Madrid pia imekuwa timu ya kwanza katika szekta ya michezo duniani kuingiza mapato yaliyovuka euro milioni 500 (Sh. trilioni 1) kwa mwaka.

Michango ya wanachama, kutokana na malipo ya ada ya kila mwaka na mauzo ya tiketi, kwa pamoja vimeichangia 9.5% ya mapato yote.

Faida waliyoingiza Real Madrid ni euro milioni 24.2 (Sh. bilioni 49), ambayo imepungua kwa 23.3% kulinganisha na mwaka wa fedha uliopita.

Kupungua huko kwa faida kumetokana na ongezeko la gharama za ulinzi, mabadiliko ya kodi na kiasi cha pesa kilichotengwa kukabiliana na kudorora kwa uchumi, pamoja na gharama zilizotokana na uwekezaji zaidi walioufanya katika majengo.

Taarifa njema zaidi kwa Real Madrid ni kwamba, deni halisi la klabu limepungua mno kwa kiasi cha 26.5%, hivyo kubaki euro milioni 124.7 (Sh. bilioni 250) tu.


Makadirio ya mapato ya Real Madrid kwa mwaka huu wa fedha (2012-13) ni euro milioni 516.6 (Sh.trilioni 1.038), huku faida inayotarajiwa ikiwa ni euro milioni 24.4 (Sh.bilioni 49).

No comments:

Post a Comment