Saturday, September 15, 2012

MSIJISUMBUE, RONALDO HAENDI MAN CITY - MOURINHO

Ronaldo

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesisitiza kuwa Cristiano Ronaldo HATAENDA Manchester City.

Mourinho anaamini kwamba straika wake nyota — ambaye amefunga magoli 150 katika mechi 149 — haendi kokote.

Alipoulizwa atafanya nini kama Man City — wapinzani wao wa Jumanne katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya — watatuma ofa ya kutaka kumsajili Ronaldo, 'The Special One' alijibu kwa utulivu: "Nitaziambia klabu zote zimsahau Cristiano.

"Msipoteze muda wenu... Cristiano na Real Madrid kila upande ndio sahihi kwa mwingine."

No comments:

Post a Comment