Sunday, September 16, 2012

PUYOL NJE WIKI 6, AUMIA GOTI JANA USIKU

Puyol akiwa na kikinga uso chake kufuatia majeraha ya kichwani yaliyomuweka nje hadi jana aliporejea na kuumia tena goti

NAHODHA wa Barcelona, Carles Puyol alipata majeraha ya goti katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Getafe juzi usiku, ambayo huenda yakamweka nje ya uwanja kwa majuma sita.

Kocha wa Barca, Tito Vilanova alisema baada ya ushindi huo: "Daima ni tatizo unapompoteza mchezaji kama yeye. Tunajua jinsi Puyol alivyo muhimu kwenye timu. Alicheza vizuri sana mechi, alileta mengi katika timu. Tunataraji atarejea haraka."

No comments:

Post a Comment