Tuesday, September 18, 2012

WENGER: NACHUKIA KUMUONA RVP KAVAA JEZI YA MAN UTD

Robin van Persie
Robin Van Persie wa Manchester United akishangilia goli la ushindi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwenye Uwanja wa St Mary's mjini Southampton, England Septemba 2, 2012. RVP alifunga 'hat-trick' katika ushindi wa 3-2.

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anahofu kwamba uhamisho wa Robin van Persie kwenda Manchester United utarejea kumshughulikia yeye mwenyewe.

Wenger anaenda na timu yake kuwakabili mabingwa wa Ufaransa Montpellier katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kesho bila ya straika wake mkali wa mwaka jana.

Van Persie alisaini kujiunga na Manchester United na Wenger amesema: "Ningependa aende kwenye klabu ya nje ya Uingereza, ili asije kutushukia.

"Inabidi ukubali, ni sehemu ya maisha. Hakika inauma kumuona akiwa amevaa jezi nyingine.

"Kila anachokifanya, hujaribu kukifanya kwa ubora wa juu.

"Unaweza kumpigia simu saa 4 usiku na huwezi kumkuta yuko kwenye klabu ya usiku.

"Pengine atakuwa anaangalia mechi ya soka, video au anajiandaa kwa mechi ijayo."

No comments:

Post a Comment