Wednesday, September 26, 2012

PEOPLE'S POWER YA WANAFUNZI YAMPONZA MKUU WA SHULE YA SEKLONDARI ILBORU... NAIBU WAZIRI KASSIM MAJALIWA AMPIGA CHINI

Kuanzia leo namsimamisha mkuu wa shule yenu... sasa rudini madarasani! Naibu Waziri wa Elimu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi waliogoma wa Shule ya Sekondari ya Ilboru jijini Arusha.
Hatimaye nguvu ya umma maarufu kama  'peoples power' imezaa matunda kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ilboru ya Arusha baada ya serikali kusikia kilio chao dhidi ya mkuu wa shule hiyo, Jovinas Mutabuzi na kuamua kumsimamisha mara moja.

Wakitumia umoja wao, wanafunzi hao ambao wana vipaji maalum walifanya maandamano mfululizo na kugoma kuingia madarasani kushinikiza kuwa mkuu huyo aondoshwe kwani amekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo yao kitaaluma kutokana na tuhuma kibao zinazomkabili; zikiwemo za kuwagawa kwa itikadi za kidini, kutimua ovyo walimu wao wazuri na pia kuwalipisha faini ya kati ya Sh. 150,000 hadi 190,000 pindi wanapokutwa na hatia kama ya makosa ya kuchelewa kurudi kutoka likizo ambapo wakati mwingine amekuwa akiwataka walipe fedha hizo kwa njia ya  M-Pesa.

Naibu Waziri wa Elimu, Kassim Majaliwa ndiye aliyemaliza migomo na maandamano ya wanafunzi hao baada ya kumsimamisha mkuu huyo wa shule (Mutabuzi) na kuagiza ucuhunguzi zaidi juu ya tuhuma dhidi yake.

Baada ya uamuzi huo, wanafunzi walishangilia na kuendelea ratiba za masomo kama kawaida.
 

No comments:

Post a Comment