Wednesday, September 26, 2012

SHARAPOVA ATINGA ROBO FAINALI TENIS TOKYO… SASA AENDELEA KUTISHA BAADA YA KUBAINI HANA UJAUZITO!
Maria Sharapova
Sharapova akiwa katika pozi la utata nje ya uwanja. 
TOKYO, Japan
MARIA Sharapova amekabiliana vyema na tatizo lake la kuanzisha mpira vibaya na kushinda leo kwa pointi 6-2 7-6 dhidi ya Lucie Safarova na kutinga robo fainali ya michuano ya tenis ya Pan Pacific Open inayoendelea jijini Tokyo, Japan.

Hata hivyo, Sharapova ambaye ni bingwa wa taji la michuano ya tenis ya French Open, alishinda kwa tabu baada ya ‘kuchemsha’ mara kadhaa katika kuanzisha mipira. 

"Baada ya mechi ya muda mrefu jana, nimejikuta nikirishishwa na ushindi huu wa seti mbili," amesema Sharapova, aliyetumia zaidi ya saa tatu kushinda dhidi ya Heather Watson jana. 

Sasa Sharapova atavaana na Samantha Stosur, ambaye pia alitinga robo fainali baada ya kushinda kwa pointi 6-4 7-5 dhidi ya Dominika Cibulkova.

Hivi karibuni, Sharapova aliyekuwa akisumbuliwa na tumbo, alisema kuwa amefurahi baada ya vipimo kuonyesha kuwa hana ujauzito na baada ya hapo akaendelea kuonyesha kiwango kizuri uwanjani.

No comments:

Post a Comment