Thursday, September 20, 2012

NI AIBU MOURINHO KUSHANGILIA KAMA TAAHIRA, ADAI MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA BARCELONA

Mourinho akishangilia kwa kuteleza kwa magoti baada ya Ronaldo kufunga goli la ushindi la Real Madrid dhidi ya Man City juzi. Real walishinda 3-2.
Mourinho akishangilia kwa kuteleza kwa magoti baada ya Ronaldo kufunga goli la ushindi la Real Madrid dhidi ya Man City juzi. Real walishinda 3-2.

MAKAMU wa rais wa zamani wa Barcelona, Alfons Godall amemuita kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho kuwa ni "taahira".

Godall alitumia ukurasa wake wa twitter baada ya kumuona Morurinho akishangilia kiwazimu goli la ushindi la Cristiano Ronaldo dhidi ya Manchester City.

Ali-tweet: "Ajabu taahira alishangilia goli kama mchezaji. Anahitaji kufidia ushangiliaji ambao aliukosa wakati akiwa mchezaji mchovu ..."

No comments:

Post a Comment