Saturday, September 15, 2012

GIGGS BADO ANA MISIMU MIWILI KUSTAAFU MAN UTD - FERGIE


'Babu' Giggs akisongesha ndani ya Man U mwaka 2012 
Handsome boy...! Hapa Giggs akiwa yosso anayetisha Man U mwaka 1992

Yosso Giggs akiwa kazini Man U ... ni mwaka 1992.

Ryan Giggs akipungia mikono mashabiki... msimu wa Ligi Kuu ya England 1992-93

Tuzo...! Machi 1992, Ryan Giggs alitwaa Tuzo ya Mwansoka Bora Chipukizi wa Mwaka wa Ligi Kuu ya England. Pichani anaonekana akiwa ameshikilia kombe la Rumbelows walilotwaa April, 1992 baada ya Man U kuwafunga Nottingham Forest.
Desemba 2009: Giggs anaonekana akiwa na Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka 2009 iliyotolewa na BBC.
Kama ana kizizi vile...! Ryan Giggs akishangilia goli lake 'kali' alilofunga katika dakika ya mwisho ya mechi na kuipa pointi Man U katika mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya Norwich City kwenye Uwanja wa Carrow Road mjini Norwich, February 26, 2012.
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amebainisha kuwa msimu ujao huenda usiwe wa mwisho kwa Ryan Giggs katika soka.

Giggs bado hajaanza katika kikosi cha kwanza msimu huu — ingawa jambo hilo linaweza kubadilika leo — na Ferguson anaamini kwamba nyota huyo wa Wales anaweza bado kuendelea kuvaa jezi ya United katika misimu miwili ijayo.

Alisema: "Ninachoona ni kwamba Ryan anaweza kucheza kwa miaka mingine kadhaa, ninapomuangalia.

"Paul Scholes ni tofauti kimwili kuliko Ryan na alikuwa na majeraha katika miaka michache iliyopita, majeraha mawili ya goti, alikuwa na majeraha ya jicho. Lakini bado amecheza mechi 700, hii ni baab'kubwa.”

No comments:

Post a Comment