Monday, September 24, 2012

MSHIKE MSHIKE WA KUSAKA TIMU YA KIKAPU MKOA WA MBEYA

Mchezaji wa timu ya kikapu ya shule ya sekondari Wenda, Gaudence Chrispine akijaribu kumtoka mwanafunzi wa shule ya seokondari Iyunga zote za jijini  Mbeya wakati wa mashindano ya kutafuta timu ya mpira wa kikapu ya Mkoa wa Mbeya kwenye viwanja vya Youth Center jijini Mbeya jana. Mashindano hao yalidhaminiwa na kampuni ya Coca Cola kupitia kinywaji chake cha Sprite.

Mchezaji wa mpira wa kikapu timu ya shule ya sekondari Wenda ya jijini Mbeya, Gasper Benedict akiondoa mpira katika eneo goli wakati wa mechi yao dhidi ya sekondari Iyunga katika mechi ya kutafuta wachezaji watakaounda timu ya kombaini ya Mkoa wa Mbeya kwenye kiwanja cha Kikatoliki cha Jijini Mbeya. Mashindano hayo yanadhaminiwa na kampuni ya Coca Cola, kupitia kinywaji cha Sprite.



No comments:

Post a Comment