Thursday, September 6, 2012

MOURINHO: MSINIULIZE KUHUSU RONALDO


Jose Mourinho
Ronaldo
Ronaldo


KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amekataa maswali kuhusu suala la Cristiano Ronaldo.

Kauli ya Ronaldo Jumapili imeziamsha klabu zinazomuhitaji za Manchester United na Manchester City.

Alipoulizwa kuhusu kinachoendelea, Mourinho aliliambia gazeti la AS: "Ni suala ambaIo sipaswi na wala sitalizungumzia. Silifahamu.

"Haya yanaonekana yatakuwa mahojiano ya aina yake. Nataka kuzungumzia kila kitu. Kuhusu maswali yenu ya awali, nimefafanua na kutoa majibu ya uwazi, lakini msiniulize maswali zaidi kuhusu Ronaldo. Mnapaswa kunielewa. Msilazimishe kwenye hili ..."

No comments:

Post a Comment