![]() |
| Jose Mourinho |
MADRID, Hispania
KOCHA Jose Mourinho wa Real Madrid amekiri hatimaye kwamba bklabu yake
imepangwa kwenye kundi gumu katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Manchester City wataanza kuivaa
Real Madrid kwenye Uwanja wa Bernabeu Septemba 18, huku mabingwa wa Bundesliga,
Ligi Kuu ya Ujerumani, Borussia Dortmund na mabingwa wa
Ligi Kuu ya Uholanzi, Ajax, pia wakiwa katika kundi hilo
la D.
Mourinho amesistiza kwamba
wachezaji wake hawatakuwa tayari kufanya makosa yoyote yale katika mechi zao
sita ngumu za kundi hilo kama watataka kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa
hatua ya 16-bora.
Ameiambia AS: "Sio
tu kwamba kuna mabingwa wa Ligi Kuu nne, bali ni mabingwa wa ligi kuu tatu kali
zaidi barani Ulaya -- zaLa Liga (Hispania), Ligi Kuu ya England na Bundesliga.
"Kwangu mimi naona
kama soka la Italia limeyumba kiasi.
"Soka la Ufaransa ni
wazi kwamba linaimarika, lakini bado halijafikia kiwango chetu.
"Ni kundi gumu sana.
"Na nyingine
inayokamilisha kundi hili ni Ajax, ambao kila mara huwa na kazi ya kujenga
upya kikosi chao lakini siku zote huonekana kuwa wazuri katika kupata wachezaji
wapya wakali, vijana ambao hulenga kujitengenezea majina na kupambana kwa lengo
hilo."

No comments:
Post a Comment