Thursday, September 6, 2012

DULLY SYKES: JINA LANGU SASA NI 'SUPER STAR"

Dully Sykes: Sasa nataka nifahamike kama Super Stars. 
Msanii wa siku nyingi wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, amesema leo kuwa sasa anataka atambulike zaidi kwa jina jipya la "Super Star".

Akizungumza katika mahojiano yake yaliyorushwa leo na kituo cha redio cha Clouds FM, Dully amesema kuwa ameamua kujiita jina hilo kwa vile ni kweli kuwa yeye ni "Super Star", na kwamba ma-super star wengi Bongo wamemkuta yeye akiwa tayari ni super star.


 Hata hivyo, akaongeza kuwa hajiiti "Mega Super Star" wala "International Super Star" kwa sababu baba yake tayari ameshakuwa na hadhi hiyo.

"Mimi nd'o Super Star kwa sababu masupa star wote wamenikuta tayari nikiwa Super Star," amesema Dully Sykes, aliyewahi kutamba na nyimbo nyingi kama "Sharifa", "Historia ya Kweli", "Hi", "Salome", "Joanita", "Sikufahamu" na "Bongofleva".

No comments:

Post a Comment