Wednesday, September 26, 2012

MOURINHO AKERWA NA MESUT OZIL KUJIRUSHA USIKU

Mesut Ozil akikimbia na mpira wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Valencia iliyomalizika kwa sare ya 1-1. Anayeonekana nyuma ni kocha Jose Mourinho.
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho ameanza kuingiwa hofu na tabia ya maisha ya kiungo wake wa kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil, hasa kuhusiana na kawaida yake ya kujirusha usiku.

Kipindi cha televisheni nchini Hispania cha Futboleros kimefichua juzi usiku kwamba kujirusha kwa Ozil usiku katika maeneo ya kula bata jijini Madrid kunampa hofu Mourinho kuwa kunaweza kuathiri kiwango cha kiungo huyo.

Tayari alishalazimika kuzungumza na Ozil kuhusiana na tabia yake hiyo miezi 12 iliyopita na sasa matatizo hayo yameibuka tena upya.

Mourinho bado anamchukulia Ozil kuwa ni miongoni mwa wachezaji wake nyota, lakini anajiandaa kumtumia zaidi Luka Modric kama kiungo-mchezeshaji wa kutumainiwa, labda mpaka Ozil atakapojirekebisha.

No comments:

Post a Comment