Sunday, September 2, 2012

MICHAEL ESSIEN ACHEKELEA MAISHA MAPYA REAL MADRID... AJIFUA NA WENZAKE, MOURINHO AMPANGA KATIKA KIKOSI KITAKACHOCHEZA MECHI YA LA LIGA DHIDI YA GRANADA LEO SAA 2:50 USIKU KWA SAA ZA KIBONGO

Karibu mwana... hapa ni makombe tu msimu huu! Essien (kulia) akichati  na Pepe (katikati) na Benzema wakati alipojinga nao mazoezini kwa mara ya kwanza mara tu baada ya utambulisho wake kwenye Uwanja wa Bernabeu jana.

Ubungo terminal? Hapa ni wakati Essien alipotua na begi lake tu jijini Madrid jana kwa nia ya kukamilisha usajili wake Real Madrid.


Karibu kijana... nakuaminia, wee bado jembe la ukweli na hapa utatisha sana! Kocha Jose Mourinho wa Real Madrid akimkaribisha Essien
Afya kwanza... baada ya kupokelewa, ilibidi Essien achukuliwe vipimo vya afya ili kujua kama kweli yuko fiti au bado ni 'kimeo' kutokana na tatizo lake la goti? Hapa anachukuliwa vipimo hivyo vya afya.

Uko fiti kiafya. Naamini kijana utatufaa sana na kutuletea makombe kama unayoyaona hapa nyuma...! Rais wa Real Madrid, Florentino Perez akimkabidhi Essien jezi yake namba 15 baada ya 'jembe' hilo kufuzu vipimo vya afya jana. 

Si mnaiona jezi yangu? Hapa Essien akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari baada ya kukamilisha usajili wake Real Madrid jana.

Nimependedha eenh...! Essien akiwa na jezi ya klabu yake mpya ya Real Madrid.
Hapa Essien akiwa kwenye Uwanja wa Real Madrid wa Bernabeu baada ya kukamilisha usajili wake klabuni hapo jana.
Maujuzi... Essien akionyesha utundu wake baada ya kutambulishwa Real Madrid jana.  
Nina usongo na hao Barcelona!

Dah... hapa raha sana! Essien (wa pili kushoto) akitaniana na wachezaji wenzake Real Madrid wakati alipoanza kujifua nao kwa mara ya kwanza jana.  Wengine ni Pepe ( kushoto), Kaka (wa pili kushoto) na Luka Modric.
Hapa upendo tu..! Essien akitaniana na wenzake kwenye mazoezi ya Real Madrid jana.
MADRID, Hispania
Kiungo wa kimataifa wa Ghana, Michael Esssien amesema kuwa amefurahi mno kukamilisha uhamisho wake wa mkopo wa muda mrefu kutoka Chelsea na kutua Real Madrid jana huku akiahidi kucheza kwa nguvu na uwezo wake wote ili kuisaidia timu hiyo kutimiza lengo la kutwaa kila taji msimu huu.

“Kuitwa na Mourinho ni zaidi ya furaha kwangu, yeye amekuwa kama baba yangu na niko tayari kucheza katika nafasi yoyote atakayoamua kunipanga; tuna uhusiano mzuri sana baina yetu”, amesema mchezaji huyo mpya wa Real Madrid, ambaye alitua Chelsea mwaka 2005 baada ya kusajiliwa na Mourinho ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa akiwaongoza mabingwa hao wa Ulaya .

Licha ya kutua jana tu na kukabidhiwa jezi namba 15, Essien alikwenda moja kwa moja mazoezini na kujifua na wenzake kabla ya kujumuishwa katika kikosi cha wachezaji 20 wa Real Madrid kitakachokuwa tayari kucheza leo saa 2:50 usiku kwa saa za Kibongo dhidi ya Granada katika mechi yao ya tatu ya msimu huu wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Wachezaji 20 waliojumuishwa kikosini na kocha Jose Mourinho leo ni:
Makipa: Casillas, Adán na Pacheco.


Mabeki: Sergio Ramos, Marcelo, Albiol, Pepe, Arbeloa na Varane.


Viungo: Özil, Xabi Alonso, Khedira, Essien, Modric, Callejón, Di María na Kaká.


Mastraika: Cristiano Ronaldo, Benzema na Higuaín.

No comments:

Post a Comment