Sunday, September 2, 2012

PODOLSKI, CAZORLA WAIPA ARSENAL USHINDI 'MTAMU' WA 2-0 DHIDI YA LIVERPOOL YA KINA GERRARD, SUAREZ, SAHIN

Dah... mkosi gani huu? Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard akiwa mwenye huzuni tele baada ya 'chama' lake kukalishwa na Arsenal mbele ya mashabiki wao kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo. 
Mtanipenda tuuuu...! Santi Cazorla wa Arsenal (kulia) akishangilia bao alilofunga dhidi ya Liverpool wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, leo Septemba 2, 2012.  (Picha: REUTERS)
Hebu tulia weweee...! Mikel Arteta wa Arsenal akichuana na Luis Suarez wa Liverpool (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, leo Septemba 2, 2012 (Picha: REUTERS)
Wee kama huujui mziki wangu waulize wenzako... ! Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal (kushoto) akichuana na Nuri Sahin wa Liverpool wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, leo Septemba 2, 2012. Sahin amesajiliwa na Liverpool kwa mkopo akitokea Real Madrid. (Picha: REUTERS)
Hapa hupiti dogo...! Mikel Arteta wa Arsenal akichuana na Joe Allen wa Liverpool (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, leo Septemba 2, 2012.  (Picha: REUTERS)
Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal (kushoto) akimfungisha tela Raheem Sterling wa Liverpool wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, leo Septemba 2, 2012.  (Picha: REUTERS)

LONDON, England
Arsenal wameanza kufanya kweli katika Ligi Kuu ya England kwa gharama za Liverpool baada ya nyota wao wapya Lukas Podolski na Santi Cazorla wote kufunga mabao yao ya kwanza tangu wajiunge kwenye klabu hiyo wakati wakishinda ugenini 'kiulaini' kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Anfield.

Sare mbili za 0-0 kufuatia mauzo ya straika Robin van Persie kwa klabu ya Manchester United ziliibua maswali kuhusiana na uwezo wa kufunga wa Arsenal lakini Podolski alijibu kwa kufunga bao safi kabla ya mapumziko na kuwapa uongozi wageni hao.

Mhispania Cazorla aliihakikishia Arsenal ushindi katika dakika ya 67 na kumuacha kocha mpya wa iverpool, Brendan Rodgers akibaki na pointi moja tu baada ya kikosi chake kucheza mechi tatu za ligi tangu atwae madaraka.

Arsenal, ambao bado hawajaruhusu goli msimu huu, wamepanda hadi katika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi tano huku Liverpool wakiendelea kuhaha katika nafasi ya nne kutoka mkiani.

No comments:

Post a Comment