Friday, September 21, 2012

MECHI YA SIMBA v YANGA KURUSHWA 'LIVE' SUPER SPORT NA MECHI NYINGINE NNE KATIKA "SUPER WEEKEND"

Luninga kubwa ya ndani ya Uwanja wa Taifa ikionyesha matokeo ya mechi ya Simba na Yanga wakatik zilipokutana kwa mara ya mwisho.

MECHI tano za Ligi Kuu ya Vodacom za Super Weekend katika mzunguko wa kwanza zitakazooneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sport zitaanza kati ya saa 11:30 jioni na saa 1 kamili usiku.

Septemba 28 mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku. Mechi ya Simba na Tanzania Prisons itakayochezwa Septemba 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 11 kamili jioni.

Yanga na African Lyon zenyewe zitapambana Septemba 30 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni wakati Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar zitaoneshana kazi Oktoba 1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.

Mechi ya mwisho katika Super Weekend itakuwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwakutanisha watani wa jadi Yanga na Simba, na itaanza kutimua vumbi saa 1 kamili usiku.

No comments:

Post a Comment