Friday, September 21, 2012

LIVERPOOL YASHINDA KWA SHIDA 5-3 EUROPA

Jonjo Shelvey akishangilia goli lake dhidi ya Young Boys jana. Liverpool walishnda 3-2.
Clint Dempsey wa Tottenham akipiga kichwa dhidi ya Lazio wakati wa mechi yao ya Ligi ya Europa dhidi ya Lazio. Timu hizo zilitoka 0-0.


JONJO Shelvey aliiokoa Liverpool kwa magoli mawili katika mechi iliyojaa ushindani ya ya hatua ya makundi ya Ligi ya Europa ugenini dhidi ya Young Boys.

Juhani Ojala alijifunga kwa kichwa na kuiweka Liverpool mbele kabla ya ulinzi mbovu kumruhusu Raphael Nuzzolo kufunga goli la kusawazisha.

Mchezaji aliyekuwa akiichezea Liverpool kwa mara ya kwanza Andre Wisdom alirejesha uongozi wa wageni kwa goli la kichwa, kabla ya Ojala kufunga kwa kichwa la kusawazisha na Gonzalo Zarate kupiga la tatu na kuwafanya Young Boys kuongoza 3-2.

Kichwa cha Sebastian Coates na Shelvey akafunga tena kuwapa Liverpool ambao walijaza yosso ushindi. Liverpool iliwapumzisha wakali wake ambao Jumapili watacheza dhidi ya Manchester United katika Ligi Kuu ya England.

Mabingwa Atletico Madrid walianza kutetea vizuri ubingwa wao Ligi ya Europa kwa ushindi mwepesi wa 3-0 dhidi ya Hapoel Tel Aviv katika mechi waliyotawala mwanzo-mwisho kwenye Uwanja wa Bloomfield jana usiku.

Magoli kutoka kwa Cristian Rodriguez, Diego Costa na Adrian Lopez ya liwapa Atletico ushindi wa kujiamini katika mechi ambayo waliwapumzisha mastaa wao kadhaa akiwamo Radamel Falcao.


TOTTENHAM SARE 0-0
Tottenham Hotspur walianza katpeni yao ya kusaka ubingwa wa Ligi ya Europa kwa sare ya bila ya magoli baada ya kubanwa na 'wasumbufu' Lazio.

Clint Dempsey alifunga kwa kichwa katika kipindi cha kwanza lakini goli lale lilikataliwa kwa kuwa alikuwa ameotea, wakati wageni waligongesha besela kupitia shuti la Alvaro Gonzalez.

Aaron Lennon na Dempsey walishindwa kufunga katika piga nikupige ya langoni mwa Lazio na Spurs wakaachwa wamefadhaika baada ya goli la kichwa la Steven Caulker lilipokataliwa kwa kuonekana akimsukuma beki kabla ya kufunga.

NEWCASTLE WASHIKILIWA
Newcastle waligongesha nguzo mara tatu wakati walipoanza kampeni zao za Ligi ya Europa kwa sare ya bila ya magoli ugenini dhidi ya Maritimo katika kisiwa cha Madeira.

Dan Gosling aligongesha nguzo kwa shuti la chini katika dakikaya 30, Shola Ameobi akagongesha besela kwa kushuti la mkunjo, baada ya mpira wake wa kichwa kusukumiwa kwenye nguzo.

Kichwa cha nguvu cha Valentin Roberge kutoka katika kona kilichookolewa na Davide Santon langoni mwa Newcastle zikiwa zimebaki dakika 10, ndio iliyokuwa nafasi ya karibu zaidi ya kufunga kwa timu hiyo ya Ureno.
.
MATOKEO YA JANA SEPT.20, 2012 - LIGI YA EUROPA

 * AEL Limassol        0 - 0 Borussia M'gladbach
 * Bordeaux               4 - 0 Club Bruges
 * Dnipro                    2 - 0 PSV Eind'ven
 * FC Copenhagen     2 - 1 Molde
 * Fenerbahce             2 - 2 Marseille
 * Hapoel Tel-Aviv    0 - 3 Atletico Madrid
 * Maritimo                0 - 0 Newcastle
 * Napoli                    4 - 0 AIK Solna
 * Plzen                     3 - 1 Academica
 * Udinese                 1 - 1 Anzhi Makhachkala
 * VfB Stuttgart        2 - 2 Steaua Buch't
 * Young Boys         3 - 5 Liverpool

No comments:

Post a Comment