Mrisho Ngassa (kulia) wa Simba akijaribu kumtoka mchezaji wa African Lyon wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
Emmanuel Okwi akimgeuza mtu... chezea Okwi wewe!? |
Kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya African Lyon katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
Kikosi cha African Lyon kilichocheza yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
Benchi la Lyon jana |
Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic (kushoto) akifuatilia wakati wa mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. |
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza Sh. 67,793,000.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, mashabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.
No comments:
Post a Comment