Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akishangilia baada ya kufunga goli lililowapa ushindi wa 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano wakati wa mechi yao ya La Liga kwenye Uwanja wa Teresa Rivero, Februari 26, 2012. |
Real Madrid wamekubali kwa mbinde kucheza mechi yao ya ugenini ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Rayo Vallecano leo kuanzia saa 2:45 usiku, ikiwa ni siku moja tu baada ya mechi yao kuahirishwa kwa sababu ya mtu asiyefahamika kukata nyaya za umeme za taa za Uwanja wa Rayo wa Vallecas na kusababisha giza.
Mechi hiyo ilikuwa ichezwe jana kuanzia saa 4:30 usiku lakini uwanja ulikuwa nusu-giza na mashabiki walikuwa bado wakisubiri nje ya milango iliyokuwa imefungwa kuwapiosha mafundi waliokuwa wakiendelea na matengenezo.
Rais wa Rayo, Raul Martin Presa amesema kuwa mtu huyo asiyefahamika amekata nyaya za baadhi ya taa na wakati tatuzo hilo lilipogundulika, hawakuweza kufanya lolote kwani tayari mechi hiyo ilishaahirishwa.
Awali, Real walisema kwamba hawataki tena kukumbana na tatizo hilo la taa za uwanjani na kupendekeza kuwa mechi hiyo ichezwe leo kuanzia saa 12:00 jioni (kwa saa za Kibongo), wakati Rayo wakisisitiza kwamba ichezwe kuanzia saa 3:00 usiku (kwa saa za Kibongo) ili kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi wa Rayo kuhudhuria.
Hata hivyo, mwishowe waendeshaji wa La Liga walikubaliana na pande zote mbili -- Real Madrid na Rayo Vallecano -- kuwa mechi hiyo ichezwe leo kuanzia saa 2:45 usiku (kwa saa za Kibongo).
Rayo wakasema kuwa tiketi zilizokatwa kwa ajili ya mechi ya jana ndizo zitakazotumika leo na kwamba, mashabiki wasioweza kuhudhuria wanaweza kuzirejesha.
No comments:
Post a Comment