Monday, September 24, 2012

BARCELONA WADAIWA KUWA SASA WAMEAMUA KUMFUNGIA KAZI NEMANJA VIDIC ILI WAMSAJILI KUTOKA MANCHESTER UNITED

Nemanja Vidic
Nahodha wa Manchester United, Nemanja Vidic amerudi tena kwenye rada za klabu ya Barcelona.

Imeripotiwa na Cadena SER kuwa Barca wameanza harakati za kumfukuzia Vidic katika kipindi hiki ambacho wameamua kumsajili beki bora wa kati.

Kocha wa Barca, Tito Vilanova ameiambia Barca kujaribu kumnasa Vidic, ingawa imeelezwa kuwa suala hilo linaweza kuchukua muda mrefu.

No comments:

Post a Comment