Tuesday, September 25, 2012

MCHUNGAJI MTIKILA AIBUKA KIDEDEA KATIKA KESI ALIYODAIWA KUMWITA RAIS KIKWETE 'GAIDI'

Mchungaji Christopher Mtikila
Mchungaji Christopher Mtikila ameibuka kidedea leo katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kuonekana kuwa hana hatia.

Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ilvin Mgeta, ndiye aliyetangaza hukumu iliyofutilia mbali kesi hiyo, akisema kwamba ushahidi uliotolewa mahakamani haukutosha kumtia hatiani Mchungaji Mtikila, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha Democratic Party (DP).

Hakimu Mgeta alisema kuwa waraka uliodaiwa kuwa wa uchochezi kutoka kwa Mtikila haukuwa na uwezo wa kumtoa rais aliyeko madarakani (Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete).

Kesi hiyo iliyounguruma kwa muda mrefu, ilivuta hisia za watu wengi na baadhi yao walijazana mahakamani leo, wakitaka kujua hatma ya Mtikila ambaye awali ilidaiwa kuwa alimkashifu Rais Kikwete kwa kumwita 'gaidi'..

No comments:

Post a Comment