Mamba aliyekamatwa Mississippi |
MAMBA mwenye uzito wa kg. 316 amenaswa kufuatia juhudi ya kumsaka iliyofanywa na watu wanne kwenye ranchi ya Mississippi nchini Marekani na ameweka rekodi ya kuwa mamba mzito zaidi nchini humo.
Eneo la chini la Mississippi Delta linahusisha klabu nyingi za uwindaji, ardhi ya mbao, kilimo na maeneo ya hifadhi za wanyama.
Rekodi ya awali nchini humo ilikuwa ni mamba mwenye uzito wa kg. 312 na alikamatwa mwaka jana kwenye maji hayo hayo ya Delta.
Mamba huyo aliyenaswa ana urefu wa futi 13 na inchi 1.5 (yaani takriban sawa na urefu wa Hasheem Thabeet WAWILI. Hasheem ana urefu wa futi 7.3).
Hata hivyo, rekodi rasmi za mamba wakubwa zaidi duniani zinashikiliwa na mamba wawili wenye urefu wa futi 20 (mita 6.2) na kg 1,200.
Mamba wa kwanza aliuawa Mto Mary kaskazini mwa Australia mwaka 1974 na kupimwa na maafisa wa wanyama. Mamba wa pili aliuawa mwaka 1983 katika Mto Fly, Papua New Guinea. Katika suala la mamba wa pili, kilichopimwa kilikuwa ni ngozi ya mamba huyo na inafahamika kwamba ngozi pekee huwa inatoa vipimo pungufu vya urefu halisi wa mnyama, hivyo mamba huyo inawezekana alikuwa na urefu wa sentimeta 10 zaidi.
No comments:
Post a Comment