Wednesday, September 26, 2012

COASTAL YAIUA KAGERA SUGAR 3-2... KOCHA MPYA WA MAKIPA JUMA PONDAMALI ADAI WALITUMIA MFUMO WA BARCELONA KUIBUKA NA USHINDI... NSA JOB APIGA 2

Coastal Union ya Tanga imeibuka na ushindi wa nyumbani wa mabao 3-2 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku kocha wao mpya wa makipa, Juma Pondamali akisema kuwa siri ya ushindi wao ni kutumia mfumo wa Barcelona wa 3-4-3

Magoli ya Coastal katika mechi hiyo yalifungwa na Daniel Hanga na Nsa Job akaongeza mengine mawili.

"Nimechukua mfumo wa Barcelona wa 3-4-3... ule wa 4-4-2 umezoeleka, nikatumia wa Barca na mambo yakawa safi," alisema Pondamali aliyeiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kutimuliwa kwa makocha wa zamani, Juma Mgunda na Habib Kondo.

Katika mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Bara leo, Polisi Moro ilishikiliwa kwa sare ya 0-0 na Toto African ya Mwanza.

No comments:

Post a Comment