Thursday, September 20, 2012

PIQUE NJE WIKI MBILI AU TATU KWA KUUMIA MGUU


Gerard Pique wa Barcelona akitoka uwanjani baada ya kuumia wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Spartak Moscow kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, jana Septemba 19, 2012.

Kipa wa Barcelona, Victor Valdes (kushoto) akimliwaza beki Gerard Pique wakati akitoka uwanjani baada ya kuumia katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Spartak Moscow kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, jana Septemba 19, 2012.

Gerard Pique wa Barcelona akitoka uwanjani baada ya kuumia wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Spartak Moscow kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, jana Septemba 19, 2012.

BARCELONA, Hispania
TATIZO la majeruhi Barcelona liliongezeka jana wakati beki wa kati Gerard Pique alipoumia mguu na sasa atakuwa nje kwa wiki mbili ama tatu.

Pique aliumia mguu wa kushoto mapema katika mechi ambayo Barca walishinda 3-2 katika Ligi ya Klabu Bingwa nyumbani dhidi ya Spartak Moscow na akaungana na beki mwenzake Carles Puyol na kiungo Andres Iniesta kwenye orodha ya majeraha.

Alirejea uwanjani baada ya kupatiwa matibabu lakini hakuweza kuendelea na nafasi yake ikachukuliwa na kiungo mpya Alex Song katika dakika ya 12.

Beki huyo wa kimataifa wa Hispania ataikosa mechi ya Barca ya La Liga nyumbani dhidi ya Granada Jumamosi na ya ugenini dhidi ya Sevilla wiki moja baadaye lakini huenda akarejea mapema kuwakabili Benfica katika Ligi ya Klabu Bingwa Jumanne Oktoba 2.

No comments:

Post a Comment