Sunday, September 9, 2012

KAMA MBWAI MBWAI... NANI ALIAMUA MAKUSUDI KUVURUGA MPANGO WA MAN UTD KUMUUZA ZENIT

Nani

NANI kwa makusudi aliamua kuharibu mpango wa Manchester United kumuuza kwa Zenit St Petersburg wili iliyopita, imebainika.

Gazeti la Mirror la Uingereza limesema kuwa winga huyo wa kimataifa wa Ureno ana hasira baada ya Man United kutaka kumuuza kwa Zenit St Petersburg katikati ya wiki bila ya ridhaa yake.

Nani alitaka mshahara wa zaidi ya paundi 200,000 kwa wiki kwa kutambua kuwa Zenit watajitoa katika mipango ya kutaka kumsajili.

Chanzo kilicho karibu na mchezaji huyo kimesema: "Haikuwa bahati mbaya kwa Nani kufanya vile. Alimweleza wakala wake adai mshahara wa kiwazimu kama Zenit wanataka kuzungumza naye. Alitarajia watakataa, lakini bado waliendelea kutaka mazungumzo.
"Mwishowe, Nani alizima simu yake na kuwaambia watu wa karibuni yake kutosema chochote kuhusu yeye kama kuna yeyote atawapigia simu.

"Hakutaka kuondoka. Ana furaha kukaa benchi na kusubiri mkataba wake umalizike aondoke bure kama Man United wataendelea kumwekea ngumu."

No comments:

Post a Comment