Saturday, September 8, 2012

MESSI ATISHA AKIIONGOZA ARGENTINA KUKAA KILELENI MWA KUNDI LA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014... MESSI SASA AMEFUNGA MAGOLI 10 KATIKA MECHI SITA ZA ARGENTINA

Straika wa Argentina, Lionel Messi (aliyeipa mgongo kamera) akifunga kwa 'fri-kiki' wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER
Winga wa Argentina, Angel Di Maria (kushoto) akishangilia pamoja na mchezaji mwenzake Lionel Messi baada ya kufunga goli dhidi ya Paraguay wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER
Straika wa Argentina, Lionel Messi (kushoto) akimuacha mchezaji wa Paraguay, Victor Caceres wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER
Straika wa Argentina, Lionel Messi (wa pili kushoto) akishangilia goli lake alilofunga wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER

Straika wa Argentina, Lionel Messi akishangilia goli lake alilofunga wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER

Straika wa Argentina, Lionel Messi akishangilia goli lake alilofunga wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER

Straika wa Argentina, Lionel Messi akishangilia goli lake alilofunga wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER

Straika wa Argentina, Gonzalo Higuain akishangilia goli lake alilofunga wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER

Straika wa Argentina, Gonzalo Higuain (kushoto) akishangilia goli lake alilofunga wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Paraguay mjini Cordoba jana usiku Septemba 7, 2012. Picha: REUTER

Messi akichanja mbunga katikati ya mabeki wawili...

Messi akichanja mbunga katikati ya mabeki wawili

Chenga kali lazima ukae... Messi akiwalamba chenga mabeki wa Paraguay

ARGENTINA ya Lionel Messi iliibwaga Paraguay 3-1 na kupanda kileleni mwa msimamo wa Kundi la Amerika Kusini la kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2014 kwenye Uwanja wa Mario Kempes usiku wa jana Ijumaa.

Magoli kutoka kwa Angel Di Maria, Gonzalo Higuain na Messi, aliyefunga kwa 'fri-kiki' ya "hatari", yaliwapa Argentina ushindi wao wa kwanza nyumbani dhidi ya Paraguay katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia katika miaka 39.

Argentina wanaongoza Kundi la Amerika Kusini wakiwa na pointi 13 kutokana na mechi sita, pointi moja juu ya Chile na Ecuador na mbili juu ya Uruguay.

Paraguay, waliofika robo-fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini 2010, wamebaki nafasi moja kutoka mkiani wakiwa na pointi nne kabla ya timu inayoshika mkia ya Peru kucheza nyumbani dhidi ya Venezuela.

Argentina walipata goli la kuongoza katika dakika ya pili wakati Ezequiel Lavezzi alipopiga krosi katikati, Higuain akamrejeshea mpira na winga huyo akampasia Di Maria aliyefunga kwa shuti la mguu wa kushoto lililokwenda kwenye kona ya juu "anapotagia ndege".

Paraguay walipata goli la bahati la kusawazisha kutokana na "counter" katika dakika ya 17 wakati kiungo wa ulinzi Rodrigo Bran, aliyecheza badala ya Javier Mascherano aliyefungiwa, kuwapa wageni penalti kwa kushika mpira ndani ya boksi.

Kiungo Jonathan Fabbro alifunga penalti hiyo iliyomshinda kipa Sergio Romero kutokana na shuti kali lililoenda kwenye kona ya juu.

Di Maria alikaribia kufunga tena kwa mpira wa kona ambao almanusura uingie moja kwa moja wavuni kutokea katika kona ya upande wa kulia aliyoipiga kwa mguu wa kushoto lakini kipa Justo Villar alifanikiwa kuupangua mpira.

Argentina walirejesha uongozi wao katika dakika ya 30 wakati Higuain alipochangamkia makosa ya mabeki upande wa kulia, akampita beki wa kushoto Richard Ortiz na kupiga shuti la chini lililomshinda kipa Villar na kutinga katika nyavu ndogo.

Messi angeweza kufunga goli la tatu muda mfupi baadaye kwa 'fri-kiki'' kutokea upande wa kushoto lakini shuti lake liligonga nguzo ya jirani.

Nahodha huyo wa Argentina angeweza kufunga tena mwanzoni mwa kipindi cha pili pale alipo alipoichana safu ya ulinzi na kuudokoa mpira juu ya kipa Villar lakini mpira ukagonga 'besela'.

Messi alirekebisha makosa yake kwa 'fri-kiki' ya "kifo" kutokea umbali wa zaidi ya mita 30 ambayo ilienda moja kwa moja kwenye wavu wa nguzo ya kushoto ya kipa Villar aliyeruka kuufuata mpira bila ya mafanikio katika dakika ya 63 na kufanya jumla ya mabao yake aliyoifungia timu yake ya taifa ya Argentina kuwa 10 katika mechi sita zilizopita.

Argentina ilikuwa haijaifunga Paraguay katika mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nyumbani tangu mwaka 1973. Mechi tano za kufuzu kwa Kombe la Dunia baina ya timu hizo tangu wakati huo zilimalizika kwa sare.

Paraguay ambao "walipaki basi" katika mechi ya jana walimsumbua kipa wa Argentina, Romero, mara chache sana na walitumbukiza mpira wavuni kutokana na 'fri-kiki' katika dakika za lala-salama lakini lilikataliwa kwa kuotea.

No comments:

Post a Comment