Monday, September 24, 2012

JOHN TERRY AMCHANGANYA KOCHA HODGSON KWA KUSTAAFU KUICHEZEA TAIFA ENGLAND

John Terry
LONDON, England
Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amekubali kwa shingo upande uamuzi wa John Terry kustaafu mechi za kimataifa lakini amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi wa beki huyo wa kati.


Terry, ambaye jana alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kumfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi mchezaji Anton Ferdinand wa Queens Park Rangers, mbele ya Chama cha Soka cha England (FA), alitangaza leo kuwa anaachana na soka la kimataifa.


"Napenda kumshukuru John Terry kwa kujitolea kwake katika timu ya taifa ya England tangu nilipoanza kuifundisha," amesema Hodgson katika taarifa yake iliyotolewa na FA.


"Nasikitika kumpoteza mchezaji wa aina ya John ambaye ana kipaji na pia uzoefu wa mechi za kimataifa,' ameongeza kocha huyo.

No comments:

Post a Comment