Thursday, September 27, 2012

KAKA APIGA HAT-TRICK KUIPA REAL MADRID USHINDI WA 8-0.. MOURINHO AMFAGILIA..ASEMA SASA 'ATAMFIKIRIA'

Kaka wa Real Madrid akishikilia tuzo yake ya kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya mchezo wao wa kuwania Kombe la Santiago Bernabeu dhidi ya Millonarios FC kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jana Septemba 26, 2012.
MADRID, Hispania
Kaka, ambaye bado hajaichezea Real Madrid katika mechi rasmi msimu huu, alionyesha sehemu ya makali aliyobaki nayo kwa kufunga magoli matatu (hat-trick) wakati klabu yake ikiibuka na ushindi wa 8-0 dhidi ya Millonarios ya Colombia katika mechi yao ya kila mwaka kuwania taji la Santiago Bernabeu jana.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, aliyeigharimu Real euro milioni 65 (Sh. bilioni 130) miaka mitatu iliyopita, anaonekana kuwa ‘mzigo’ katika kikosi cha kocha Jose Mourinho ambacho humtumia Mesut Ozil na mchezaji mpya, Luka Modric katika nafasi ya kiungo mchezeshaji.

"Kaka amecheza vizuri sana, kama ilivyokuwa kwa timu nzima," Mourinho aliuambia mkutano na waandishi wa habari.


"Kaka na wachezaji wengine wameonyesha kiwango cha juu sana na kumfanya kocha awafikirie."

Kaka alianza katika kikosi dhaifu na kufunga mabao matatu, moja likiwa ni la penati, wakati Real ikiibuka na ushindi.

Kiungo huyo mwenye miaka 30 ameshindwa kufikia matarajio yaliyokuwapo kwake na ameonyesha sehemu tu ya kiwango chake cha zamani kutokana na kuandamwa na majeraha ya kila mara tangu alipotua Real Madrid miaka mitatu iliyopita akitokea AC Milan.

No comments:

Post a Comment