Friday, September 14, 2012

HATUNA HAJA YA OWEN, TUNAYE STERLING - RODGERS

Yosso mwenyekipaji wa Liverpool, Raheem Sterling
Raheem Sterling

Raheem Sterling

Raheem Sterling wa Liverpool (kushoto) akiwania mpira dhidi ya Alex Oxlade-Chamberlain wa Arsenal wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool Septemba 2, 2012.

Michael Owen akijifua baada ya kujiunga na Stoke City

KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesisitiza kwamba hakuwahi kufikiria kumrejesha Michael Owen klabuni hapo.

Owen, aliyetemwa na Manchester United, amejiunga na Stoke City wiki iliyopita kwa mkataba wa mwaka mmoja.

"Liverpool haikumfikiria Michael Owen," Rodgers aliiambia Talksport. "Kama tumeshindwa kupata watu tuliowahitaji katika kipindi cha usajili, niliamua kwamba nitabaki na nilionao.

"Hakuna sababu ya kuweka pesa katika kuimarisha shule yetu ya soka kisha hatuwapi nafasi vijana wadogo. Angalia mchango uliotolewa na Raheem Sterling ilhali ndio kwanza ana umri wa miaka 17. Nilichompa ni fursa tu na ameichangamkia.

"Tuna wachezaji wengi vijana na natumai katika miezi ijayo tutawaona na kuangalia kwa namna gani wanang'aa."

No comments:

Post a Comment