Saturday, September 15, 2012

FABREGAS KUFULIA NILAUMIWE MIMI - VILANOVA

Fabregas

KOCHA wa Barcelona, Tito Vilanova amesema yeye ndiye wa kulaumiwa kufuatia kushuka kwa kiwango cha Cesc Fabregas.

Hatma ya Cesc klabuni Barcelona imekuwa mjadala kutokana na kuanza vibaya msimu.

"Yeye ni mchezaji wa kiwango cha dunia ambaye anaingia katika timu yoyote duniani," kocha huyo mwenye umri wa miaka 42 aliliambia gazeti la AS la Hispania.

"Hapa Barca, imetokea kwamba anahitaji kugombea namba na wachezaji ambao wamekuwa bora duniani katika miaka ya karibuni katika nafasi zao.

"Sikubaliani na mitazamo kwamba Cesc hachezi vizuri. Makocha ni lazima pia walaumiwe. Kama sitaweza kuchimba kipaji chake, huwezi kumlaumu tu mchezaji - ni lazima nilaumiwe na mimi pia."

No comments:

Post a Comment