Saturday, September 22, 2012

GUTI: CRISTIANO RONALDO ANASTAHILI KUONYESHWA UPENDO REAL MADRID

Ronaldo
MADRID, Hispania
Mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Guti ameizungumzia hali ya Cristiano Ronaldo kwenye klabu hiyo, akisema kwamba madai ya hivi karibuni ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kuwa hana furaha ni lazima yanatokana na masuala mengine binafsi na wala siyo "ishu" ya pesa.

Guti mwenye miaka 35, alifunga magoli 46 katika mechi 387 alizocheza akiwa na mabingwa hao wa Hispania kabla ya kuhamia Besiktas mwanzoni mwa msimu wa 2010-11.

"Kama (Ronaldo) hana furaha, sababu haitakuwa masuala ya pesa, itakuwa ni kutokana na jambo jingine binafsi," mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania amewaambia waandishi wa habari. 


"Labda anachohitaji ni kuona anaonyeshwa zaidi upendo, kitu ambacho wakati fulani wote huwa tunakihitaji."

No comments:

Post a Comment