Sunday, September 23, 2012

CASILLAS: NDIO SIKUSHANGILIA GOLI LA RONALDO

Casillas
Ronaldo akishangilia goli lake dhidi ya Manchester City ambalo Casillas hakulishangilia

Mourinho akishangilia kwa kuteleza kwa magoti baada ya Ronaldo kufunga goli la ushindi la Real Madrid dhidi ya Man City. Real walishinda 3-2.

KIPA wa Real Madrid, Iker Casillas ametoa sababu iliyomfanya asishangilie goli la ushindi la Cristiano Ronaldo dhidi ya Manchester City katika mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Casillas amesema hakushangilia kwaajili ya kumuenzi Dawid, mtoto wa Poland aliyefariki Jumanne ambaye alikutana naye wakati wa fainali za Mataifa ya Ulaya.

Kocha wa Real, Jose Mourinho, ambaye goli hilo lilimpagawisha hadi akashangilia kwa kuteleza kwa magoti kama wafanyavyo wachezaji  alisema: "Kila mmoja anapokea kivyake matokeo kwa sababu zake. Kuna magoli muhimu ambayo hata hayaninyanyui kwenye siti yangu na katika goli hili nililipokea kama nilivyolipokea. Kilichomuhimu ni kufunga, kushinda na kutimiza malengo makuu. Kila mmoja alikuwa na furaha sawa kwa kushinda mechi."

No comments:

Post a Comment