Wednesday, September 26, 2012

GODBLESS LEMA AFURAHIA KESI YAKE KUSIKILIZWA NA JAJI MKUU CHANDE

Jaji Mohamed Othman Chande
Godbless Lema
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia Chadema, Godbless Lema amesema kuwa anaamini Mahakama ya Rufaa itapitia vyema vipengele vya kesi iliyompoka ubunge wake na kutoa uamuzi wa haki kwavile anamuamini Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande.

Akizungumza katika mahojiano yake leo na kituo cha redio cha Clouds FM kupitia kipindi cha Bongo Amplifanya, Lema amesema kuwa yeye binafsi hataki kupendelewa bali haki itendeke na kwamba anaamini kuwa uamuzi wa jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa litakaloongozwa na Jaji Chande utakuwa ni wa haki na yuko tayari kuupokea.

"Sitaki upendeleo, nipendelewa nitaogopa, nitalia... niko tayari  kurudi kwenye uchaguzi, na ninaamini nitashinda kwa idadi ya kura za kubebwa kwenye canter.... nimefurahi kuwa kesi hii itaongozwa na Jaji Mkuu Chande," amesema.

'Yeye (Chande) ndiyo mkuu wa mahakama... ninaamini vipengele vitapitiwa kwa haki," amesema Lema ambaye ubunge wake ulitenguliwa na mahakama kutokana na kasoro kadhaa na hivyo akakata rufaa kupinga uamuzi huo

No comments:

Post a Comment