Saturday, September 15, 2012

MOURINHO: SIJALI RONALDO AKIWA HANA RAHA, AKICHEZA VIZURI KWANGU INATOSHA

Ronaldo

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amesisitiza hachanganyikiwi kuhusu hali ya Cristiano Ronaldo.

Ronaldo atacheza mechi yao ya ugenini dhidi ya Sevilla leo saa 5:00 usiku siku kadhaa baada ya kudai kwamba "hana raha" klabuni Real.

Mourinho alisema: "Mimi ni mwalimu wa soka na kwa sasa jambo pekee ninaloangalia ni kuona timu yangu inaendelea kucheza vizuri.

"Kama Cristiano hana furaha na akacheza kama ninavyotaka acheze, basi hiyo ni poa kwangu.

"Cristiano anafanya kazi kwa asilimia 100, anacheza kwa asilimia  100. Wakati mwengine anafanya mara nyingine vibaya. Hawezi kuleta matokeo ya ushindi katika kila mechi lakini daima ni mchezaji wa kushirikiana na timu, ambaye katika mazoezi kuhusu suala la nidhamu ni baab'kubwa.

"Sihofii kuhusu mambo ya ziada ambayo si ya msingi kazini."

Mourinho pia aliviasa vyombo vya habari kumhukumu Ronaldo kutokana na kiwango chake na sio kuvumisha kuhusu mambo mengine.

"Nadhani nyie (vyombo vya habari) mmekuwa na siku 15 za kuvumisha kwa sababu hapajakuwa na mechi yoyote ama mechi muhimu za kimataifa.

"Hivi sasa Cristiano anahitaji amani na utulivu ili kucheza soka, ambalo anajua kwamba ndilo analolipenda zaidi.

"Nyie, watu wa Bernabeu na jamii, tunapaswa kupima kiwango chake uwanjani na si zaidi ya hilo.

"Kama kesho (leo) katika dakika 75 au 80 atakuwa amecheza soka bovu, au amechoka, basi atapumzishwa na mwingine ataingia, iko hivyo tu."

No comments:

Post a Comment