Sunday, September 9, 2012

FERGIE: NILETEENI CRISTIANO RONALDO

Ronaldo
Ronaldo
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akiugulia baada ya kuchezwa madhambi wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Granada kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Septemba 2, 2012. Rinaldo alitoka baada ya rafu hiyo na baada ya mechi aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hana furaha.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akiugulia baada ya kuchezwa madhambi wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Granada kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Septemba 2, 2012. Rinaldo alitoka baada ya rafu hiyo na baada ya mechi aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hana furaha.

SAF akiwa na Ronaldo uwanjani
Sir Alex Ferguson akiwa na Ronaldo mazoezini

Sir Alex Ferguson akiwa na Ronaldo kwenye mkutano na waandishi wa habari
Cristiano Ronaldo na kocha Sir Alex Ferguson wa Manchester United wakipozi na tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Mwaka iliyotwaliwa na Ronaldo kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya England baina ya Manchester United na Wigan Athletic kwenye Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester, England Januari 14, 2009.
Cristiano Ronaldo (kushoto) akicheka na Sir Alex Ferguson wakati wakihudhuria upangaji wa makundi la Ligi ya Klabu Bingwa ya Ulaya kwa msimu wa 2008/2009 kwenye ukumbi wa Grimaldi Center mjini Monte Carlo, Monaco Agosti 28, 2008.
Ngoja nami nikuonyeshe maujuzi... kocha Sir Alex Ferguson wa Manchester United akimiliki mpira huku Cristiano Ronaldo akishuhudia wakati wa mazoezi ya Manchester United yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Rome, Italia Machi 31, 2008. Manchester United ilikuwa ikijiandaa kuikabili Roma katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kesho yake mjini Rome.

SIR Alex Ferguson atawaomba wamiliki wa klabu ya Manchester United wavunje benki ili kumrejesha Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.

Gazeti la Sunday Mirror limesema Ferguson atawaomba Manchester United kulipa chochote kinachotakiwa ili kumrejesha Ronaldo Old Trafford.

Hivi sasa SAF anataka kujua kama ni kweli straika huyo wa Ureno amedhamiria kutaka kuondoka Real Madrid.

Miaka mitatu tu iliyopita Ronaldo alijiunga na Real katika ada ya uhamisho iliyoweka rekodi ya dunia ya paundi milioni 80 akitokea Man United.

Hivi sasa, kama ni kweli anataka kuondoka, ­Ferguson ataiomba familia ya Glazer – ambayo inamiliki klabu ya Man United – kufanya kila iwezalo ili kumsajili tena straika huyo mwenye umri wa miaka 27.

Chanzo kutoka ndani ya Man United kilisema: "Kocha aliweka wazi wakati Ronaldo alipojiunga na Real kwamba kama ataondoka Bernabeu arudi Old Trafford.

"Ni uhamisho ambao utathibitisha kwamba Man United bado inaweza kupambana na yeyote kwa majina makubwa katika soka.

"Lakini, kwa sasa, ni Ronaldo tu anayejua kama yuko 'siriasi' kuhusu kuondoka Madrid au anawazingua tu."

No comments:

Post a Comment