Saturday, September 22, 2012

FERGIE: LIVERPOOL MSIMFUKUZE KOCHA BRENDAN RODGERS

Sir Alex Ferguson
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akiwa hoi wakati timu yake ikiadhibiwa na Arsenal wakati wa mechi ya ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool Septemba 2, 2012.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers akiwa hoi wakati timu yake ikiadhibiwa na Arsenal wakati wa mechi ya ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool Septemba 2, 2012.
Andre Villas-Boas

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema  Brendan Rodgers anahitaji muda Liverpool.

Baadhi tayari wameanza kuhoji kama kocha huyo mwenye umri wa miaka 39 ni mtu sahihi wa kushikilia ajira hiyo yenye changamoto.

Inamkumbusha Ferguson hali aliyojikuta Andre Villas-Boas klabuni Chelsea. Na haikumalizika vyema kwa Mreno huyo.

"Kocha yeyote kijana anahitaji muda lakini katika soka la sasa hupati kitu kama hicho," alisema Ferguson. "Muangalie Villas-Boas klabuni Chelsea msimu uliopita. Alikuwa kijana mdogo ambaye alidumu kwa miezi saba tu.

Ferguson amesema Rodgers ameanza kwa wakati mgumu kama yeye alipotua Manchester United, lakini mafanikio yamekuja baada ya kupewa muda.

No comments:

Post a Comment