Monday, September 17, 2012

BABA YAKE TUNDU LISSU ALIYEFARIKI MUHIMBILI JANA JIONI KUAGWA TEGETA ALHAMISI


Mhe. Tundu Lissu
BABA wa Mhe. Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, Mzee Lissu, ataagwa Alhamisi ijayo nyumbani kwa mbunge huyo, Tegeta jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Singida.

Akizungumza jioni hii, Tundu Lissu alisema kuwa baba yake alifariki dunia jana saa 11:00 jioni kwenye Hospitali ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.

“Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwangu Tegeta na ataagwa Alhamisi,” amesema Tundu Lissu.

No comments:

Post a Comment