Friday, September 14, 2012

CAPELLO: BAADA YA MESSI NI FALCAO

Falcao wa Atletico Madrid akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Barcelona wakati wa mechi yao ya La Liga kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Hispania Februari 26, 2012.
Lionel Messi


KOCHA wa timu ya taifa ya Urusi, Fabio Capello ni shabiki mkubwa wa straika wa Atletico Madrid, Radamel Falcao.

Capello anamuweka Falcao katika daraja moja na straika wa Barcelona, Lionel Messi.

"Katika maisha yangu yote ya soka, kuna mchezaji mmoja tu ambaye amenikosha kama Messi pale nilipomuona kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yangu ya Juventus katika kuwania kombe la Joan Gamper, na huyo ni Radamel Falcao," Capello aliliambia gazeti la michezo la Italia la Gazzetta dello Sport.

No comments:

Post a Comment